Tarehe 15 mwezi wa kenda: Siku kuu ya u-democrasia ulimwenguni

16 sep 2015

Tarehe 15 mwezi wa kenda: Siku kuu ya u-democrasia ulimwenguni

Martin Kobler, Kiongozi wa MONUSCO na Jose Maria Aranaz, Muwakilishi wa Kiongozi ahusikaye na kugombeya haki za binadamu na zile za ki-siasa pamoja na uhuru kwa wote

Kinshasa, tarehe 15 mwezi wa kenda mwaka wa 2015. «Siku kuu ya u-democrasia ulimwenguni kote ni siku ya lazima kubwa sana kwa jamhuri ya kidemocrasia ya Congo yenye kutayarisha uchaguzi katika siku za usoni. Kwa kufikiria hatuwa hiyo, ni vema kuheshimu kanuni mbalimbali sawa vile kupatia nafasi upinzani na shirika la raia."

Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo yenye kukaliwa na watu millioni 75 wakiwemo vijana wengi, inamatatizo mengi sana ajili ya kufikiriya maendeleo yake ya kudumu na uongozi bora. Ingawa serikali na vyama mbalimbali vya ki-siasa vinajitoleya kuhudumia, mchango wa shirika la raia nao pia ni wa manufaa makubwa katika kipindi hiki maalum ajili ya kuboresha maisha ya wakaaji na maendeleo yak i-uchumi. Kinyume ni kwamba, serekeli inapashwa kuchukuwa fursa hii ya mchango wa shirika la raia ajili ya kuruhusu wakaaji wote watolee mchango wao katika uwezekano wa kuinuwa maisha nchini kote. MONUSCO pamoja na Umoja wa mataifa kwa ujumla vinaendelea kuhudumia jamhuri ya kidemocrasia ya Congo kukiwekovile vile mchango mwengine kutoka kwa washiriki wengine katika juhudi za kuhimarisha udemocrasia na kufikiria lengo la maendeleo ya kudumu.

"Katika matayarisho ya kipindi cha uchaguzi nchini humu, Maria Jose Aranaz alisema kwamba ni vema kuheshimu haki za binadamu na zile za kisiasa, ni muhimu pia kutolea nafasi ya mazungumzo kwa wote, kuacha huru miungano ya vyama vya upinzani wajitetee na kuendesha mikutano yao bila vikwazo, ni vema pia vyombo vya habari na miungano ya shirika la raia vitumike bila kunyanyaswa, bila woga wa kushtakiwa na mtu yeyote yule.

Jambo kwa waandishi:

Mwezi wa kenda mwaka wa 1997, kongamano la wanabunge wa ulimwengu liitwalo (UIP) limetangaza hatuwa muhimu kuhusu udemocrasia ulimwenguni kote. Hatuwa hiyo hiyo inatiya mkazo juu

ya ginsi udemocrasia unaopashwa kuendeshwa na viongozi wa serikali kufwatana na mwelekezo unaofwatwa katika maeneo mengine za ulimwengu nzima.

Kufwatana na masilahi ya kongamano hilo la wanabunge wenye kujumuhika katika muungano wa UIP, rarehe 15 mwezi wa kenda unaitwa tarehe ya kutangazwa kwa kibaruwa cha kutetea udemocrasia ulimwenguni kote. Hatuwa hiyo inaitwa sasa Msaada kwa juhudi za serikali ajili ya kuhimarisha udemocrasia mupya kulingana na makubaliano ya umoja wa mataifa ya tarehe 8 mwezi wa kumi na moja munamo mwaka wa 2007.

*Traduit par Pascal Masirika Bisimwa